Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 527

Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بِن مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ العَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الوَالِدَيْنِ» قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ» قَالَ: حَدَّثَنِي بِهِنَّ، وَلَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِي.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu" Akasema: Alinihadithia mambo hayo, na lau ningemtaka ziada angenizidishia.

English translation

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: I asked the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him): Which deed is dearest to Allah? He said: "Offering prayer at its earliest appointed time." I said: Then, what comes next? He said: "Dutifulness to one's parents." I said: Then, what comes next? He said: "Jihad in the way of Allah." He said: These were the things he said to me, and if I had asked him for more, he would have given me more.

Maelezo

Aliulizwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu?. Akasema: Ni swala za faradhi katika wakati wake uliopangwa na sheria, Kisha wema kwa wazazi wawili, kwa kuwafanyia wema, na kusimamia haki zao, na kuacha kuwaasi, kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitetea dini ya Uislamu na waislamu, na kudhihirisha alama zake, na hii inakuwa kwa nafsi na mali. Akasema bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake: Alinieleza amali hizi; na lau kama ningelimwambia: Kisha ipi? Basi angenizidishia.

Faida

  • Kuzidiana kwa amali kati yake ni kulingana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa amali hiyo.
  • Himizo kwa muislamu katika kupupia amali bora kisha inayofuata kwa ubora.
  • Kutofautiana kwa majibu ya Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhusu amali bora kulingana na watu na hali zao, na kulingana na lenye manufaa mengi kwa kila mmoja miongoni mwao.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)