Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ لَقِيَ اللهَ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ لَقِيَهُ يُشْرِكُ بِهِ دَخَلَ النَّارَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni".
English translation
Jābir ibn ‘Abdullāh (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) say: "Whoever meets Allah without associating partners with Him will enter Paradise, and whoever meets Him while associating partners with Him will enter Hellfire."
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika Pepo hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake, nakuwa atakayekufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote atabakizwa milele Motoni.
Faida
- Ubora wa tauhidi, nakuwa ni sababu ya kuokoka na kukaa milele Motoni.
- Ukaribu wa Pepo na Moto kwa mja nakuwa hakuna baina yake na hivyo viwili isipokuwa kifo.
- Tahadhari inatolewa ya kujiepusha na ushirikina mdogo au mkubwa, kwa sababu kuokoka na moto ni kwa kuuepuka.
- Mazingatio katika matendo huangaliwa mwisho wake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.