Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رسولَ اللهِ صلي الله عليه وسلم قال: «لَو يُعطَى النّاسُ بدَعواهُم لادَّعَى رِجالٌ أموالَ قَومٍ ودِماءَهُم، لَكِنَّ البَيِّنَةَ على المُدَّعِى، واليَمينَ على مَن أنكَرَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mweyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti wangelipewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
English translation
Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Were people to be given everything they claimed, some men would claim the properties and blood of other people. However, the onus of proof is on the plaintiff, and the oath is upon the one who denies the claim (defendant)."
Maelezo
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.
Faida
- Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na hadithi hii ni msingi katika misingi ya utoaji wa hukumu, na ni marejeo makubwa wakati wa mzozo na ugomvi.
- Sheria imekuja kulinda mali za watu na damu zao zisichezewe.
- Hakimu asikuhumu kwa elimu yake bali arudi katika ushahidi.
- Yeyote atakayedai madai ambayo hayana uthibitisho yatakataliwa, iwe yanahusu haki na miamala au masuala ya imani na sayansi.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.