Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-66511

Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَمِيرِ المُؤْمِنِينَ أَبِي حَفْصٍ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إنَّمَا الأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ، وَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيَا يُصِيبُهَا أَوْ امْرَأَةٍ يَنْكِحُهَا فَهِجْرَتُهُ إلَى مَا هَاجَرَ إلَيْهِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa kiongozi wa waumini Abuu Hafsi Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi (malipo yake yatakuwa) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ataipata, au kwa ajili ya mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa lile alilolihamia".

English translation

The Commander of the Believers, Abu Hafs ‘Umar ibn al-Khattāb (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (ﷺ) say: "Verily, the reward of deeds depends on intentions, and each person will be rewarded according to what he intended. So, he whose emigration is for the sake of Allah and His Messenger, his emigration will be for the sake of Allah and His Messenger, and he whose emigration is to achieve some worldly gain or take some woman in marriage, his migration will be for what he has migrated for."

Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.

Faida

  • Himizo la kuwa na Ikhlasi (kutakasa nia) kwani Mwenyezi Mungu hakubali katika matendo isipokuwa yale yatakayokusudiwa kupata radhi zake.
  • Matendo ambayo hutumika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwayo, akiyafanya muislamu mtu mzima kwa njia ya mazoea hawezi kuwa na thawabu juu yake, mpaka akusudie kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo hayo.
  • Nia inatofautisha baina ya ibada na ibada nyingine na vile vile ibada na mazoea.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)