Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 241

Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرٍو رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: رَجَعْنَا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ مَكَّةَ إِلَى الْمَدِينَةِ حَتَّى إِذَا كُنَّا بِمَاءٍ بِالطَّرِيقِ تَعَجَّلَ قَوْمٌ عِنْدَ الْعَصْرِ، فَتَوَضَّؤُوا وَهُمْ عِجَالٌ، فَانْتَهَيْنَا إِلَيْهِمْ وَأَعْقَابُهُمْ تَلُوحُ لَمْ يَمَسَّهَا الْمَاءُ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَيْلٌ لِلْأَعْقَابِ مِنَ النَّارِ أَسْبِغُوا الْوُضُوءَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina mpaka tulipofika katika njia yenye maji, walifanya haraka baadhi ya watu kusali laasiri, wakatia udhu wakiwa na haraka, tukawakuta na hali yakuwa visigino vyao vikiwa vyeupe havijaguswa na maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".

English translation

‘Abdullāh ibn ‘Amr (may Allah be pleased with him) reported: We returned with the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) from Makkah to Madīnah, and when we came to some water on the way, some of the people were in a hurry at the time of the ‘Asr prayer and performed ablution hurriedly; and when we reached them, their heels were dry, and no water had touched them. Thereupon, the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Beware of negnot washing your heels properly, for not doing so can lead to them being burnt in the Hellfire! So, perform your ablution thoroughly."

Maelezo

Alisafiri Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina akiwa pamoja na Masahaba zake, wakiwa njiani walipata maji, wakaenda mbio kutia udhu kwa ajili ya swala ya Alaasiri baadhi ya Masahaba, mpaka ukaonekana weupe mwisho wa miguu yao kwa mtu mwenye kuitazama kwa kukosa maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ni adhabu na maangamivu katika moto kwa wenye kufanya uzembe wa kuosha mwisho wa nyayo wakati wa udhu, na akawaamrisha wapitilize katika kuukamilisha udhu.

Faida

  • Ulazima wa kuosha miguu miwili katika udhu; kwa sababu lau kama ingefaa kufuta asingetoa ahadi ya adhabu ya moto kwa mwenye kuacha kuosha mwisho wa miguu yake.
  • Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vyenye kuoshwa wakati wa udhu, nakuwa atakayeacha sehemu ndogo ambayo ni ya wajibu kusafishwa kwa makusudi au kwa uzembe, basi swala yake haisihi.
  • Umuhimu wa kumfundisha asiyejuwa na kumuelekeza.
  • Msomi anatakiwa kukemea anayoyaona ikiwemo kupoteza wajibu na sunna, lakini kwa usulubu mzuri.
  • Amesema Muhammad Is-haqa Al-Dahalawi: Kueneza maji kuna aina tatu: Lazima (Faradhi) Nako ni kueneza maji mahali unapoosha kwa mara moja, na sunna: Nayo nikuosha kiungo mara tatu, na inapendeza: kurefusha mahali unapoosha ikiwa ni pamoja na kufanya hivyo mara tatu.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)