Historia na Wasifu wa Mtume ﷺ
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-66303

Jambo la kwanza alilioanza kupewa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika wahyi, ni njozi nzuri (za kweli) usingizini

Maisha ya Mtume na Maswahaba

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْها أَنَّهَا قَالَتْ: أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ الوَحْيِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلَّا جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ -وَهُوَ التَّعَبُّدُ- اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ العَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ المَلَكُ فَقَالَ: اقْرَأْ، قَالَ: «مَا أَنَا بِقَارِئٍ» قَالَ: «فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، قُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، فَقُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: {اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ}»، [العلق:1-3] فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، فَقَالَ: «زَمِّلُونِي، زَمِّلُونِي» فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الخَبَرَ: «لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي» فَقَالَتْ خَدِيجَةُ: كَلَّا وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الكَلَّ، وَتَكْسِبُ المَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الحَقِّ، فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ العُزَّى، ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ، وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الكِتَابَ العِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ، فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ: يَا ابْنَ عَمِّ، اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: يَا ابْنَ أَخِي، مَاذَا تَرَى؟ فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَبَرَ مَا رَأَى، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى، يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَوَ مُخْرِجِيَّ هُمْ؟»، قَالَ: نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلَّا عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا. ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ، وَفَتَرَ الوَحْيُ.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Jambo la kwanza alilioanza kupewa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika wahyi, ni njozi nzuri (za kweli) usingizini. Akawa haoti njozi isipokuwa itatokea, mfano wa mapambazuko ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga peke yake katika pango la Hira, akawa akitawa huko - ambako ni kuabudu - kwa siku kadhaa, kabla ya kurejea katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kutosha kwa ajili ya hilo, kisha alikuwa akirudi kwa Khadija na kumpatia chakula mfano wa hicho, mpaka ukweli ukamjia akiwa ndani ya pango la Hira, Malaika akamjia, akasema: "Soma!" akasema: “Mimi si msomaji.” Akanichukua na akanifunika mpaka nikachoka, kisha akaniacha, akasema: "Soma!" Nikasema: “Mimi sio msomaji". Basi akanichukua na akanifunika mara ya pili mpaka nikapatwa na uchovu, kisha akaniacha, kisha akasema: "Soma!" nikasema: "Mimi si msomaji", basi akanichukua na akanifunika kwa mara ya tatu, kisha akaniacha, na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Alaq: 1-3] Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akarudi huku moyo wake ukitetemeka, akaingia kwa Khadija binti Khuwailidi, Allah amuwiye radhi, na akasema: “Nisaidieni, kuwa pamoja nami, Nisaidieni, kuwa pamoja nami” Basi wakamkumbatia mpaka hofu ikamtoka, basi akamwambia Khadija na kumueleza habari hiyo: “Nilihofia sana nafsi yangu" Khadija akasema: Hapana, Wallahi kamwe Mwenyezi Mungu hatokufedhehesha, hakika wewe utaunga udugu, utamsaidia mnyonge, na utaleta kilichokosekana, na utamkirimu mgeni, na utasaidia wakati wa matatizo ya haki, basi Khadija akaondoka naye mpaka wakafika kwa Waraqa bin Nawfal bin Asad bin Abdil-Uzza, binamu yake Khadija, na alikuwa ni mtu aliyeingia katika Ukristo wakati wa kabla ya Uislamu, na alikuwa akiandika vitabu vya Kiebrania, hivyo aliandika kutoka katika Injili kwa Kiebrania, kiasi alichotaka Mwenyezi Mungu akiandike, alikuwa mzee ambaye amekwisha pofuka, basi Khadija akamwambia: Ewe binamu, sikia kutoka kwa mtoto wa ndugu yako. Waraqa akamuuliza: Ewe mpwa wangu, unaona nini? Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza aliyoyaona. Waraqa akamwambia: Hii ndiyo sheria aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa. Hakika ninatamani ningekuwa hai wakati watu wako, pindi watakapokufukuza watu wako. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Hivi, kwani watanifukuza!?" Akasema: "Ndiyo" Kamwe hakuwahi kuja mtu na kitu kama ulichokuja nacho, isipokuwa alitendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanifikia nikiwa hai, basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha Waraqa hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, na wahyi ukasimama kuteremka kwa muda.

English translation

‘Ā’ishah, Mother of the Believers, (may Allah be pleased with her) reported: The first thing the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) started to experience from the revelation was the good vision in his sleep. He never saw a vision except that it came true like the break of dawn. Then seclusion was endeared to him, and he used to retreat to the Cave of Hirā’, where he would engage in Tahannuth-which is worship—for several nights before returning to his family and taking provisions for this. He would then go back to Khadījah to take provisions again for a similar number of nights until the truth came to him while he was in the Cave of Hirā’. The Angel came to him and said: Read! He said: "I do not know how to read." He said: "He took hold of me and pressed me forcefully until I could no longer bear it and then released me, saying: Read! I said: I do not know how to read. He took hold of me and pressed me forcefully for the second time until I could no longer bear it and then released me, saying: Read! I said: I do not know how to read. He took hold of me and pressed me forcefully for the third time and then released me, saying: {Read in the name of your Lord Who created, created man from a clinging clot. Read, and your Lord is the Most Generous.}" [Surat al-‘Alaq: 1-3] The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) returned with these while his heart was trembling. He entered upon Khadījah bint Khuwaylid (may Allah be pleased with her) and said: "Cover me! Cover me!" They covered him until the shock of fear was gone from him. Then he informed Khadījah of what had happened and said to her: "Indeed, I feared for myself." Khadījah said: No, by Allah, Allah will never fail you. Verily, you maintain kinship ties, help those in need, support the destitute, provide the guests with food and shelter, and assist those affected by calamities. Khadījah took him to her cousin Waraqah ibn Nawfal ibn Asad ibn ‘Abdul-‘Uzza, who had embraced Christianity in the pre-Islamic period and used to write the Scripture in Hebrew. He would write from the Gospel in Hebrew as much as Allah wished him to write. He was an old man and had lost his eyesight. Khadījah said to him: O my cousin, listen to what your nephew has to say. Waraqah said to him: O my nephew, what have you seen? The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) informed him of what he had seen. Waraqah said to him: This is the same Nāmūs (i.e., the angel) whom Allah had sent to Moses. I wish I were young and could live until the time when your people would drive you out. The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Would they drive me out?" Waraqah said: Yes. No one has ever come with something like what you have brought without being treated with hostility. If I should live until that day, I would support you strongly. Soon after, Waraqah passed away, and the revelation paused.

Maelezo

Ameeleza mama wa Waumini, Aisha, Allah amuwiye radhi, kwamba jambo la kwanza aliloanziwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni njozi za kweli usingizini, akawa haoti kitu katika njozi zake isipokuwa kilitokea wazi mfano wa nuru ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga, na alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akifanya ibada kwa siku kadhaa, kabla ya kurudi katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kumtosheleza, kisha anarejea kwa mama wa waumini Khadija radhi za Allah ziwe juu yake, anachukua tena chakula cha kutosha idadi ya siku kama hizo, mpaka ikamjia amri ya kweli, naye akiwa katika pango la Hira. Kisha akamjia Malaika Jibril amani iwe juu yake, akamwambia: Soma, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mimi si mzuri katika kusoma, anasema: Akanishika akanibana mpaka nikachoka na kuishiwa nguvu, kisha akaniachia na kusema: Soma. Nikasema: Mimi si mzuri katika kusoma, basi akanichukua na kunibana kwa mara ya pili mpaka nikachoka na kuishiwa nguvu, kisha akaniacha, akasema: Soma. Nikasema: Sijui kusoma, basi akanichukua na akanifunika mara ya tatu, kisha akaniacha na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. Kamuumba mwanadamu kutokana na pande la nyama. Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Qalaq: 1-3]. Akarejea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na aya kadhaa, lakini kifua chake kilikuwa kikitetemeka kwa kuhofia kifo, akaingia kwa mkewe mama wa waumini Khadija binti Khuwailidi radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Nifunikeni na nguo, nifunikeni na nguo, wakamfunikwa kwa nguo mpaka hofu ikamuondokea, akasema kumwambia Khadija na akampa habari ya kilichotokea, na akasema: Nilihofia kifo juu ya nafsi, Khadija akasema: Si hivyo, Wallahi hawezi kukufedhehesha Mwenyezi Mungu kamwe! Hakika wewe utaunga udugu, na utamsaidia mnyonge ambaye jambo lake halina muelekeo, na utamnyanyua fakiri asiye na kitu; kiasi ambacho utawapa watu yale wasiyoyapata kwa asiyekuwa wewe, na utamkirimu mgeni, na utasaidia kutatua matatizo ya haki. Khadija akamchukua mpaka akamfikisha kwa Waraqa bin Naufali bin Asadi bin Abdil -Uzza, ambaye ni mtoto wa ami yake, na alikuwa ni mtu aliyeachana na mila za kale na akawa mkristo, na alikuwa akiandika kutoka katika Injili kwa lugha ya Kiebrania kiasi alichokitaka Mwenyezi Mungu akiandike, na alikuwa ni mzee mtu mzima aliyepofuka macho yake, Khadija akasema kumwambia: Ewe mtoto wa ammi, hebu msikilize mtoto wa ndugu yako, Waraqa akasema kumwambia: Ewe mtoto wa ndugu yangu, umeona nini? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamueleza habari ya kile alichokiona, Waraqa akasema kumwambia: Huyo ni Malaika Jibrili aliyemteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa amani iwe juu yake, natamani lau ningekuwa wakati huo ni kijana mwenye nguvu, laiti kama nitakuwa hai, wakati wakikufukuza watu wako, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi, kwani wao watanifukuza?!. Akasema: Ndiyo, kamwe hajawahi kuja mtu na mfano wa hiki ulichokujanacho isipokuwa aliudhiwa na kutendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanikuta nikiwa hai basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha hakukaa muda mrefu Waraqa akawa amefariki, na wahyi ukachelewa kuteremka tena kwa muda kidogo.

Faida

  • Hapa kumebainishwa mwanzo wa wahyi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Njozi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni miongoni mwa aina za wahyi.
  • Sheria ya kuchukua akiba ya mahitaji, na kwamba hilo haliendi kinyume na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwani alilifanya hilo mbora wa wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.
  • Ukamilifu wa ukarimu wake Aliyetakasika na kutukuka, kwa sababu aliwafundisha waja wake wasiyoyajua, na akawahamisha kutoka katika giza la ujinga kwenda katika nuru ya elimu.
  • Fadhila za kujua kuandika; kwa sababu ndani yake kuna manufaa makubwa yasiyohesabika; kwani kwa hilo elimu zimaendikwa, na hukumu zikawekewa mipaka, na habari za wa mwanzo zikadhibitiwa, na vikahifadhiwa vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyoteremshwa, na yakanyooka mambo ya dini na dunia.
  • Maneno ya mwanzo kuteremka katika Qur'ani ni "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba" [Al-Alaq: 1].
  • Tabia njema na mambo ya kheri ni sababu ya kusalimika na majanga mabaya, na aina mbalimbali za kero, zitakayekithiri kheri zake basi utakuwa mzuri mwisho wake, na unatarajiwa kwake usalama wa dini na dunia.
  • Hapa inaonyesha kuwa; inafaa kumsifia mtu mbele yake kukiwa na masilahi.
  • Ni wajibu kumliwaza aliyepatwa na mambo ya kuogofya, na kumpa habari njema, na kumueleza sababu za kusalimika na hilo.
  • Ushahidi mkubwa na uthibitisho ulio wazi kabisa wa ukamilifu wa Khadija, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na ukubwa wa rai yake, na nguvu ya nafsi yake, na ukubwa wa elimu yake ya kisheria, ni kwamba katika maelezo yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikusanya kila aina ya msingi wa wema, na muhimili wake, kwa sababu wema ima uwe kwa ndugu wa karibu, au kwa watu baki, au uwe kwa mwili, au kwa fedha, au kwa mwenye jukumu, au uwe kwa mtu mwingine, na alipanua mazungumzo yake katika hilo kwa ni mahali panapofaa kufanya hivyo, kwa ajili ya mlolongo wa maneno mengine.
  • Mtu yeyote atakayefikwa na jambo, inapendeza amueleze mtu anayemuamini katika nasaha zake na rai yake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)