Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ»، قِيلَ: وَمَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «الَّذِي لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَايِقَهُ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abuu Shuraihi radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake".
English translation
Abu Shurayh (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "By Allah, he does not believe. By Allah, he does not believe. By Allah, he does not believe." It was said: Who, O Messenger of Allah? He said: "The one whose neighbor is not safe from his evils."
Maelezo
Aliapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akasisitiza kiapo chake mara tatu, akasema: Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Maswahaba wakamuuliza: Na ni nani ambaye hawezi kuamini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani anahofia usaliti wake na dhulma zake na shari zake.
Faida
- Kukanushwa imani kwa yule ambaye jirani yake hapati amani kutokana na dhulma zake na shari zake hili linaonyesha kuwa ni katika madhambi makubwa, na kwamba mfanyaji wake anaupungufu wa imani.
- Himizo la msisitizo juu ya kumtendea wema jirani na kuacha kumuudhi kwa kauli au kitendo.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.