Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَشْكُرُ اللَّهَ مَنْ لَا يَشْكُرُ النَّاسَ»
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu"
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (ﷺ) said: "He who does not thank people in fact does not thank Allah."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kwa kawaida hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu kwa wema na mazuri waliyomfanyia, na hii ni kwa sababu mambo haya mawili yote yanaungana, kiasi kwamba katika tabia yake na desturi yake ni kukufuru neema na kuacha kushukuru, pia atakuwa katika kawaida yake ni kukufuru neema za Mwenyezi Mungu na kupuuza katika kushukuru kwa neema hizo.
Faida
- Umuhimu wa kuwashukuru watu kwa mazuri.
- Mneemeshaji halisia ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na viumbe ni sababu, huileta Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa amtakaye, na kwa hivyo kuwashukuru watu ni miongoni mwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kuwashukuru watu kwa wema ni dalili ya ukamilifu wa tabia njema.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.