Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 2626

Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ أَصَابَ حَدًّا فَعُجِّلَ عُقُوبَتَهُ فِي الدُّنْيَا فَاللَّهُ أَعْدَلُ مِنْ أَنْ يُثَنِّيَ عَلَى عَبْدِهِ العُقُوبَةَ فِي الآخِرَةِ، وَمَنْ أَصَابَ حَدًّا فَسَتَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ وَعَفَا عَنْهُ فَاللَّهُ أَكْرَمُ مِنْ أَنْ يَعُودَ فِي شَيْءٍ قَدْ عَفَا عَنْهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera, na atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, Mwenyezi Mungu akamsitiri na akamsamehe, basi Mwenyezi Mungu ni mkarimu zaidi (hawezi) kurudi katika jambo ambalo alikwishalisamehe".

English translation

‘Ali (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever commits a Hadd (legally punishable sin) and his punishment is hastened for him in this world, then Allah is too just to repeat the punishment for His slave in the Hereafter. And whoever commits a Hadd but Allah concealed it for him and pardoned him, Allah is too generous to retract something He has pardoned."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayefanya dhambi zinazohitaji adhabu ya kisheria, kama vile uzinzi au wizi, na akapata adhabu hiyo na ikatekelezwa duniani, basi adhabu hiyo itamfutia dhambi hiyo na kumuondolea adhabu ya Akhera. Hii ni kwa sababu Allah ni mkarimu na mwenye rehema, na hawezi kumuhukumu mja wake kwa adhabu moja mara mbili. Na ikiwa Allah amemsitiri mja wake duniani na hakumuhukumu kwa dhambi hiyo, na akamsamehe na kumghufiria, basi Allah Mtukufu ni mkarimu na mbora zaidi hawezi kurudi katika adhabu ya dhambi aliyoisamehe na kuifuta."

Faida

  • Ukubwa wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake na rehema yake.
  • Kutekeleza adhabu za kisheria katika dunia hufuta dhambi.
  • Atakayetumbukia katika dhambi ambalo ndani yake ni lazima ajisitiri na kujificha kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, na afanye haraka kufanya toba ya kweli.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)