Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ، وَتَقْلِيمِ الْأَظْفَارِ، وَنَتْفِ الْإِبِطِ، وَحَلْقِ الْعَانَةِ، أَلَّا نَتْرُكَ أَكْثَرَ مِنْ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً.
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini.
English translation
Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: A time limit was set for us regarding trimming the mustache, clipping the nails, plucking the armpit hair, and shaving the pubic hair—that we should not leave them for more than forty nights.
Maelezo
Aliweka kikomo Mtume rehema na amani ziwe juu yake cha mtu kupunguza sharubu, na kupunguza kucha za mikono na miguu, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, kusizidi kuziacha kwake zaidi ya siku arobaini.
Faida
- Amesema Shaukani: Kilicho sawa nikuwa adhibiti kwa arobaini aliyoidhibiti kwayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake haitakiwi kuivuka, na haitochukuliwa kama kwenda kinyume na sunna kwa kuacha kupunguza na mfano wake baada kurefuka mpaka ifike kikomo cha muda huo.
- Amesema bin Hubaira: Hadithi hii ndio kikomo cha kuchelewesha hilo, na kilichobora ni kulitekeleza hilo kabla ya ukomo huo.
- Uislamu umetilia kipaumbele usafi na kujitwaharisha na kujipamba.
- Kupunguza sharubu, kwa kunyoa nywele zinazoota juu ya mdomo wa juu.
- Kukwapua nywele za kwapa, kwa kuondoa nywele zinazoota humo, nayo ni sehemu inayokuwa chini ya maungio kati ya mkono na bega.
- Kunyoa nywele za siri, nazo ni nywele zinazoota pembezoni mwa tupu ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.