Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 2739

Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ عَمْرِو بْنِ الحَارِثِ خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخِي أُمِّ المؤمِنين جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الحَارِثِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُم، قَالَ: مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلَّا بَغْلَتَهُ البَيْضَاءَ، وَسِلاَحَهُ، وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Amri bin Harithi shemeji yake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kaka yake na mama wa waumini Juwairia binti Harithi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema: Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.

English translation

‘Amr ibn al-Hārith, the brother-in-law of the Messenger of Allah (ﷺ) and the brother of the Mother of the Believers, Juwayriyah bint al-Hārith (may Allah be pleased with them), reported: The Messenger of Allah (ﷺ) did not leave behind at his death a single dirham or dinar, nor a male or female servant, nor anything else—except his white mule, his weapon, a piece of land—which he declared as charity.

Maelezo

Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha Dirham ya fedha wala Dinari ya dhahabu, wala mtumwa mmilikiwa wala kijakazi mmilikiwa, wala mbuzi wala ngamia wala chochote katika mali, isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akimpanda, na silaha yake aliyokuwa akiibeba, na kipande cha Ardhi alichokitoa wakfu kwa ajili ya wasafiri.

Faida

  • Manabii hawarithiwi.
  • Kumebainishwa alivyoviacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada ya kifo chake.
  • Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha kitu chochote cha msingi, kutokana na ukarimu wake na utoaji wake na wema wake.
  • Amesema Al-Karmani: Dhamiri katika kauli yake "na akavifanya" hii inarudi katika vitu vitatu: Yaani; nyumbu na silaha na Ardhi na si katika Ardhi peke yake.
  • Shemeji: Ni kaka wa dada, na neno "Akhtani" hutumika kwa ndugu wa mwanamke.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)