Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 810

Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَابِعُوا بَيْنَ الحَجِّ وَالعُمْرَةِ، فَإِنَّهُمَا يَنْفِيَانِ الفَقْرَ وَالذُّنُوبَ كَمَا يَنْفِي الكِيرُ خَبَثَ الحَدِيدِ، وَالذَّهَبِ، وَالفِضَّةِ، وَلَيْسَ لِلْحَجَّةِ الْمَبْرُورَةِ ثَوَابٌ إِلاَّ الجَنَّةُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo".

English translation

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Perform Hajj and ‘Umrah in succession, for they expel poverty and sins just as the bellows expels impurities from iron, gold, and silver. There is no reward for an accepted Hajj except Paradise."

Maelezo

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka karibu kati ya kutimiza ibada ya Hija na ibada ya Umra, na kutoacha kuzitekeleza hali yakuwa kuna uwezo, kwa sababu kuzitekeleza kwake inakuwa ni sababu ya kuondoa umasikini na madhambi na athari zake ndani ya moyo, kama ambavyo mpulizo wa moto huwa sababu ya kuondoa uchafu wa chuma na vyote vinavyochanganyika nacho katika madini ambayo si chuma.

Faida

  • Fadhila za kufuatanisha baina ya Hija na umra na himizo katika hilo.
  • Kufuatanisha kati ya Hija na Umra ni miongoni mwa sababu za utajiri na msamaha wa madhambi.
  • Amesema Al-Mubaarakafuriy: (Huondoa umasikini) Yaani: Huuondosha kabisa, na hii inategemea maana zote mbili: Umasikini unaoonekana kwa kupatikana utajiri wa mkononi, na umasikini wa ndani, kwa kupata utajiri wa moyo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)