Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sunan an-Nasa'i · Na. HE-65613

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن سعد بن عبادة رضي الله عنه أنه قال: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أُمَّ سَعْدٍ مَاتَتْ، فَأَيُّ الصَّدَقَةِ أَفْضَلُ؟، قَالَ: «الْمَاءُ»، قَالَ: فَحَفَرَ بِئْرًا، وَقَالَ: هَذِهِ لِأُمِّ سَعْدٍ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Sa'di bin Ubada radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama Sa'di amefariki, ni sadaka ipi bora ya kumfanyia? Akasema: "Maji" Akasema: tukachimba kisima, na akasema: Kisima hiki ni kwa ajili ya mama Sa'di.

English translation

Sa‘d ibn ‘Ubādah (may Allah be pleased with him) reported that he said: "O Messenger of Allah, ’Umm Sa‘d died. Which charity is the best?" He said: 'Water.' He said: So, he dug a well and said: "This is for ’Umm Sa‘d."

Maelezo

Alifariki mama Sa'di bin Ubada radhi za Allah ziwe juu yake, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni aina ipi bora ya sadaka ili aitoe kwa niaba ya mama yake? Akamueleza rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa sadaka bora ni maji, akachimba kisima na akakifanya kuwa sadaka kwa ajili ya mama yake.

Faida

  • Kumeelezwa kuwa maji ndio sadaka bora zaidi.
  • Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Sa'di katika sadaka ya maji; kwa sababu ndio inamanufaa mapana katika mambo ya dini na dunia, na kwa sababu ya joto kali na haja ya watu na uchache wa maji.
  • Hii ni dalili kuwa malipo ya sadaka yanawafikia maiti.
  • Wema wa Sa'di bin Ubada kwa mama yake radhi za Allah ziwe juu yao.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)