Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهُ صلَّى اللهُ عليهِ وَسَلَّم: «لَقِّنُوا مَوْتَاكُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah".
English translation
Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (ﷺ) said: "Remind those of you who are dying of: La ilāha illallāh (There is no god but Allah)."
Maelezo
Anatuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Tuseme na turudie neno la kumpwekesha "Laa ilaah illa llaah" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kufikwa kwake na tabu za kifo mpaka aliseme, ili liwe neno lake la mwisho.
Faida
- Sunna ya kumtamkisha aliyefikwa na mauti.
- Inachukiza kukariri sana kumtamkisha aliyefikwa na umauti, na kumlazimisha endapo atalitamka, au ikafahamika kuwa ametamka; ili wasimsumbue akatamka maneno yasiyofaa.
- Amesema Nawawi: Na akilitamka mara moja basi asilikariri tena isipokuwa kama atatamka baada yake maneno mengine, hapo litarudiwa tena ili liwe neno lake la mwisho.
- Hadithi inakusanya kuhudhuria mbele ya aliyefikwa na umauti ili kumkumbusha na kumliwaza na kumfunga macho na kusimamia haki zake.
- Si sheria kumtamkisha mtu baada ya kifo na kaburini baada ya mazishi; kwa sababu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutolifanya hilo.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.