Historia na Wasifu wa Mtume ﷺ
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-65411

Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri

Maisha ya Mtume na Maswahaba

Kiarabu

عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى الفَجْرَ جَلَسَ فِي مُصَلَّاهُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ حَسَنًا، وَقَالَ: كَانَ لَا يَقُومُ مِنْ مُصَلَّاهُ الَّذِي يُصَلِّي فِيهِ الصُّبْحَ أَوِ الغَدَاةَ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ، فَإِذَا طَلَعَتِ الشَّمْسُ قَامَ، وَكَانُوا يَتَحَدَّثُونَ فَيَأْخُذُونَ فِي أَمْرِ الجَاهِلِيَّةِ، فَيَضْحَكُونَ وَيَتَبَسَّمُ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Jabiri bin Samura radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri, na akasema: Alikuwa hanyanyuki kutoka katika mswala wake alioswalia hapo Alfajiri au asubuhi, mpaka linapochomoza Jua, basi linapochomoza Jua anasimama, na walikuwa wakizungumza wanajikuta wameingia katika mazungumzo ya zama za ujinga, wanacheka na yeye anatabasamu.

English translation

Jābir ibn Samurah (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (ﷺ), when he performed the Fajr prayer, would remain seated in his prayer place until the sun rose brightly. He said: He would not leave the spot where he prayed Fajr or the Morning prayer until the sun had risen. When the sun rose, he would stand up. During that time, the people would talk about matters from the pre-Islamic days of ignorance; they would laugh and he would smile.

Maelezo

Na miongoni mwa sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza kwa kunyanyuka, na alikuwa hasimami kutoka katika mswala wake aliouswalia Alfajiri, mpaka Jua lichomoze. Jua linapochomoza anasimama, na walikuwa wakizungumza wanachukua katika baadhi ya mambo yao ya kabla ya Uislamu na huku yeye kanyamaza, wanacheka, na huenda yeye akatabasamu pamoja nao.

Faida

  • Sunna ya kufanya dhikiri asubuhi mpaka Jua lichomoze, na kubaki katika kikao chake anapokuwa hana udhuru.
  • Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa tabia njema na upole, kiasi kwamba alikuwa akikaa na Maswahaba zake, na akisikiliza mazungumzo yao na simulizi zao, na anatabasamu kwa sababu yake.
  • Inafaa kufanya mazungumzo na kukumbushia enzi za ujinga msikitini.
  • Inafaa kucheka na kutabasamu; kwa sababu kilichokatazwa ni kukithirisha kucheka.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)