Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنْ عَبْدَ اللهِ بْنِ عَمْرٍو رَضيَ اللهُ عَنْهُمَا يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ لَقِيَ اللهَ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا لَمْ تَضُرَّهُ مَعَهُ خَطِيئَةٌ، وَمَنْ مَاتَ وَهُوَ يُشْرِكُ بِهِ لَمْ يَنْفَعْهُ مَعَهُ حَسَنَةٌ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha".
English translation
‘Abdullah ibn ‘Amr (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (ﷺ) said: "Whoever meets Allah without associating anything with Him, no sin will harm him along with it; and whoever dies while associating partners with Him, no good deed will benefit him along with it."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekufa na akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa na tauhidi hamshirikishi na chochote basi huyo ni katika watu wa Peponi, hata kama akiadhibiwa kwa dhambi motoni, na atakayekufa huku akimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote hakuna jema lolote litakalomnufaisha; na Pepo kwake ni haramu.
Faida
- Tahadhari dhidi ya ushirikina, na kwamba hilo ni katika madhambi na makosa makubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu haisamehe.
- Fadhila ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kwamba hilo linawajibisha kuingia Peponi; hata ikiwa baada ya kuadhibiwa.
- Umuhimu wa kudumu katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu mpaka kufa, na kutofanya kinyume chake ambacho ni ushirikina.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.