Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-65049

Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ النَّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ الْأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «ضَرَبَ اللهُ مَثَلًا صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا، وَعَلَى جَنْبَتَيْ الصِّرَاطِ سُورَانِ، فِيهِمَا أَبْوَابٌ مُفَتَّحَةٌ، وَعَلَى الْأَبْوَابِ سُتُورٌ مُرْخَاةٌ، وَعَلَى بَابِ الصِّرَاطِ دَاعٍ يَقُولُ: أَيُّهَا النَّاسُ، ادْخُلُوا الصِّرَاطَ جَمِيعًا، وَلَا تَتَعَرَّجُوا، وَدَاعٍ يَدْعُو مِنْ فَوْقِ الصِّرَاطِ، فَإِذَا أَرَادَ يَفْتَحُ شَيْئًا مِنْ تِلْكَ الْأَبْوَابِ، قَالَ: وَيْحَكَ لَا تَفْتَحْهُ، فَإِنَّكَ إِنْ تَفْتَحْهُ تَلِجْهُ، وَالصِّرَاطُ الْإِسْلَامُ، وَالسُّورَانِ: حُدُودُ اللهِ، وَالْأَبْوَابُ الْمُفَتَّحَةُ: مَحَارِمُ اللهِ، وَذَلِكَ الدَّاعِي عَلَى رَأْسِ الصِّرَاطِ: كِتَابُ اللهِ، وَالدَّاعِي مِنِ فَوْقَ الصِّرَاطِ: وَاعِظُ اللهِ فِي قَلْبِ كُلِّ مُسْلِمٍ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kapokea kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka ,na pambizoni mwa njia kuna kuta mbili, kuta hizo zina milango ilikuwa wazi, na kwenye milango kuna pazia isiyomuonesha mwenyekupita, na mbele ya kila mlango kuna mwenye kuita akisema: Enyi watu, ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na juu ya huyu muitaji kuna muitaji mwingine akiita juu ya njia, na kila mja anapotaka kufungua kidogo milango hiyo anasema: Ole wako wacha usiufungue mlango huo, ikiwa utaufungua tu hutoweza kujizuia, na njia hapa ni Uislamu, na kuta mbili: Ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na milango iliyofunguliwa: Ni maharamisho ya Mwenyezi Mungu, na huyo muitaji aliyopo mwanzo wa mlango ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muitaji aliyepo juu: Ni Mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu."

English translation

An-Nawwās ibn Sam‘ān al-Ansāri (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Allah has given a parable: a straight path that is surrounded by two walls on both sides, with several open doors within the walls covered with curtains. There is a caller on the gate of the path who says: 'O people, enter the path, all of you, and do not deviate from it.' Meanwhile, a caller from above the path is also warning any person who wants to open any of these doors: 'Woe unto you! Do not open it, for if you open it, you will pass through.' The path is Islam, the two walls are the limits set by Allah, and the open doors are Allah's prohibitions. The caller on the gate of the path is the Book of Allah, while the caller above the path is Allah's admonishment in the heart of every Muslim."

Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa Mwenyezi Mungu alitolea mfano wa Uislamu na njia iliyonyooka pana isiyokuwa na konakona, na pambizoni mwa njia hii kuna kuta mbili zimeizunguka njia hii katika pande zake mbili, na njia hizo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, katikati ya hizi kuta mbili kuna milango iliyofunguliwa, na hiyo milango ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, na katika milango hiyo kuna mapazia ambayo humzuia mwenye kupita kumuona aliye ndani, na mwanzo wa njia kuna mwenye kuita akielekeza watu na kuwaongoza na akiwaambia: Ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na huyu mwenye kuita ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na juu ya njia kuna muitaji mwingine, na huyu muitaji humkemea kila mwenye kutembea katika njia hii ambaye anaelekea kutaka kufunua pazia za milango hiyo humkemea na kumwambia Ole wako usiufungue mlango huo! kwa hakika ukiufungua mlango huo utaingia na wala hutoweza kuizuia nafsi yako isiingie humo, na huyu mwenye kuita ni mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu.

Faida

  • Uislamu ndiyo Dini ya kweli, na ndiyo njia iliyonyooka ambayo hutufikisha peponi.
  • Ni wajibu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kuchunga yale aliyoyahalalisha na yale aliyoyaharamisha, na kuyapuuzia hayo kunapelekea maangamivu.
  • Ubora wa Qur'ani tukufu, na kuhimizwa kuifanyia kazi, kwakuwa ndani yake kuna muongozo, mwanga na mafanikio.
  • Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwa namna alivyoweka kwenye nyoyo za waumini kitu ambacho kinawazuia na kuwapa mawaidha ya kuwaepusha kuingia kwenye maangamivu.
  • Mwenyezi Mungu kwa huruma zake amewawekea waja wake kizuizi kinachowazuia kutumbukia kwenye maasi.
  • Miongoni mwa nyenzo za kufundishia ni kupiga mifano ili kuliweka jambo karibu na kuliweka wazi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)