Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2653

Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «كَتَبَ اللهُ مَقَادِيرَ الْخَلَائِقِ قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِخَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، قَالَ: وَعَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."

English translation

‘Abdullāh ibn ‘Amr ibn al-‘Ās (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) say: "Allah decreed the destinies of the creatures fifty thousand years before He created the heavens and the earth." He said: "when His Throne was upon the water.”

Maelezo

Anatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.

Faida

  • Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari.
  • Na Kadari: Ni ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa kujua vitu vyote na kuviandika na kutaka kwake viwe na kuviumba.
  • Kuamini kuwa mipango ya Mwenyezi Mungu (Kadari) ilikwisha andikwa kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi kunaleta tija ya kuridhika na kujisalimisha na kukubali.
  • Kwa hakika Arshi ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)