Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 2222

Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ المَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "By the One in Whose Hand my soul is, the son of Mary will soon descend among you as a just judge. He will break the cross, kill the pig, and abolish Jizyah (protection tax imposed on non-Muslims living under Muslim rule), and the wealth will be abundant to such an extent that no one will accept it."

Maelezo

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya ukaribu wa kuteremka Issa mwana wa Mariam amani iwe juu yake ili ahukumu baina ya watu kwa uadilifu na kwa sheria ya Muhammadi. nakuwa atavunja misalaba wanayoitukuza wakristo, nakuwa Issa amani iwe juu yake ataua nguruwe, Na pia amani iwe juu yake ataweka kodi (Jizia) na atawaamrisha watu wote kuingia katika Uislamu. Nakuwa mali itaenea na hatoikubali yeyote; na hii ni kwa sababu ya wingi wake, na kwa kutosheka kila mmoja na kile anachokimiliki mkononi mwake, na kuteremka kwa baraka na heri nyingi zenye kufuatana.

Faida

  • Kumethibitishwa kuteremka kwa Issa amani iwe juu yake zama za mwisho, nakuwa tukio hilo ni katika alama za Kiyama.
  • Sheria ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haitofutwa na sheria yoyote.
  • Kuteremka kwa baraka katika mali zama za mwisho, na watu kutoipenda.
  • Habari njema ya kubakia kwa dini ya Uislamu kiasi ambacho Issa amani iwe juu yake atawahukumu watu zama za mwisho.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)