Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «مَثَلُ الْمُنَافِقِ، كَمَثَلِ الشَّاةِ الْعَائِرَةِ بَيْنَ الْغَنَمَيْنِ تَعِيرُ إِلَى هَذِهِ مَرَّةً وَإِلَى هَذِهِ مَرَّةً».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Mfano wa mtu mnafiki, ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga baina ya makundi mawili ya Mbuzi, wakati mwingine huwa na kundi hili na wakati mwingine huwa na kundi lile."
English translation
Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "The hypocrite is like a ewe which goes to and fro between two flocks: going once to one and another time to the other."
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hali za wanafiki, na kuwa mnafiki ni kama Mbuzi mwenye kutangatanga na asiyejua afuate kundi gani la Mbuzi, wakati mwingine huenda kundi hili na wakati mwingine huenda na kundi lingine, Wanafiki hutangatanga baina ya imani na ukafiri, hivyo hawapo na waumini kwa wazi wazi wala kwa kujificha, wala hawapo na makafiri kwa wazi wala kwa kujificha, bali kwa muonekano wa nje wanaonekana wapo na waumini, na kwa ndani (kwa siri) wapo kwenye shaka na kutanga tanga, wakati mwingine, na wakati mwingine wanaelemea kwa hawa na wakati mwingine kwenye kundi hili.
Faida
- Miongoni mwa miongozo ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kupiga mfano ili kufahamu haraka.
- Kuweka wazi hali za wanafiki za kutangatanga kuwa na mashaka na kutokuwa na utulivu.
- Kuchukua tahadhari kutokana na hali za wanafiki na kuhimizwa kuwa na imani nje na ndani.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.