Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى رُخَصُهُ، كَمَا يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى عَزَائِمُهُ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya".
English translation
Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Allah loves that His dispensations be taken as He loves that His obligations be observed."
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu anapenda ziendewe ruhusa zake ambazo ameziweka, ikiwemo kufanya wepesi katika hukumu na ibada, na kufanya wepesi kwenye ibada kwa aliyekalifishwa na sheria ikiwa ni kwa dharura- kama vile kupunguza swala na kuikusanya wakati wa safari. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda yafanywe mambo yake ya wajibu, kwa sababu amri ya Mwenyezi Mungu katika kufuata ruhusa na kutekeleza wajibu yote ni sawa.
Faida
- Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kuwa yeye Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu anapenda ruhusa yake ifanyiwe kazi.
- Ukamilifu wa sheria hii, na kuondosha kwake uzito kwa waislamu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.