Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 214

na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، ابْنُ جُدْعَانَ كَانَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ يَصِلُ الرَّحِمَ، وَيُطْعِمُ الْمِسْكِينَ، فَهَلْ ذَاكَ نَافِعُهُ؟ قَالَ: «لَا يَنْفَعُهُ، إِنَّهُ لَمْ يَقُلْ يَوْمًا: رَبِّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."

English translation

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: I said: "O Messenger of Allah, Ibn Jud‘ān used to uphold kinship ties and feed the poor during the Jāhiliyyah (pre-Islamic era of ignorance). Will this benefit him?" He said: "It will not benefit him, for he did not ever say: My Lord, forgive my sins on the Day of Judgment."

Maelezo

Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu Abdullahi Bin Jad'aan, na alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kikuraishi kabla ya Uislamu, Na miongoni mwa vitendo vyake vizuri ni kuwa yeye: huunganisha ndugu zake na huwafanyia wema, na hulisha chakula masikini, na mambo mengine mengi ambayo Uislamu umeyahimiza kuyafanya, nakuwa matendo haya hayatomfaa katika Akhera yake; Na hilo ni kwa sababu ya kumkufuru Mola wake, na kuwa yeye hajawahi hata siku moja kusema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi makosa yangu siku ya Kiyama.

Faida

  • Kuweka wazi utukufu na ubora wa imani, na kuwa imani ni sharti la kukubaliwa matendo yote.
  • Kuweka wazi ubaya wa ukafiri, na kuwa ukafiri huporomosha matendo mema.
  • Makafiri hayatawafaa matendo yao huko Akhera kwa sababu ya kutokumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.
  • Matendo ya mwanadamu akiwa bado yupo kwenye ukafiri huandikiwa atakapo silimu na atalipwa kwa matendo hayo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)