Hadithi na Sunnah za Mtume ﷺ
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 2664

Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu

Umuhimu wa Kufuata Sunnah

Kiarabu

عن المقدام بن معدِيْكَرِب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَلَا هَلْ عَسَى رَجُلٌ يَبْلُغُهُ الْحَدِيثُ عَنِّي وَهُوَ مُتَّكِئٌ عَلَى أَرِيكَتِهِ فَيَقُولُ: بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ كِتَابُ اللهِ، فَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَلَالًا اسْتَحْلَلْنَاهُ، وَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَرَامًا حَرَّمْنَاهُ، وَإِنَّ مَا حَرَّمَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا حَرَّمَ اللهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".

English translation

Al-Miqdām ibn Ma‘dikarib (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Lo! Soon a Hadīth from me will be conveyed to a man, while he is reclining on his couch, and he says: ‘Between us and you is Allah’s Book. So, whatever we find in it that is lawful, we consider lawful, and whatever we find in it that is unlawful, we consider unlawful.’ Indeed, whatever the Messenger of Allah made unlawful, it is the same as what Allah made unlawful."

Maelezo

Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Kuitukuza Sunna kama inavyotukuzwa Qur'ani tukufu na kuhukumu kwayo.
  • Kumtii Mtume ndiyo kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi Mtume ndiyo kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kuthibitika kuwa Sunna ni hoja, na jawabu kwa mwenye kuikataa Sunna au kuipinga.
  • Na mwenye kuipinga Sunna na kudai kuwa Qur'ani pekee yamtosha, basi mtu huyo atakuwa kavipinga vyote viwili, na ni muongo kwa kudai kwake kuifuata Qur'ani.
  • Miongoni mwa alama za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake-, ni kutoa taarifa ya kitu kuwa kitatokea mbeleni na hutokea kama alivyotoa taarifa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)