Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 15

Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن جابر رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَرَأَيْتَ إِذَا صَلَّيْتُ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ، وَصُمْتُ رَمَضَانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلَالَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ؟ قَالَ: «نَعَمْ»، قَالَ: وَاللهِ لَا أَزِيدُ عَلَى ذَلِكَ شَيْئًا.

Tafsiri ya Kiswahili

Hadithi imepokelewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: "Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu, na wala sikuzidisha zaidi ya hayo je nitaingia peponi?Akasema: "Ndiyo", Akasema mtu yule: "Namuapia Mwenyezi Mungu sizidishi zaidi ya matendo hayo kitu chochote".

English translation

Jābir (may Allah be pleased with him) reported: A man said to the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him): "Do you think that if I perform the obligatory payers, fast Ramadan, treat the lawful as lawful, and treat the unlawful as unlawful, and do not do anything else beyond that, will I enter Paradise?" He said: 'Yes.' He said: "By Allah, I will not do anything more than that."

Maelezo

Anaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.

Faida

  • Muislamu kupupia juu ya kufanya mambo yaliyo faradhishwa na kuacha yaliyoharamishwa, na yawe malengo yake ni kuingia peponi.
  • Umuhimu wa kufanya yaliyo halali na kuamini uhalali wake, na kuharamisha yaliyo haramu na kuamini uharamu wake.
  • Kufanya yaliyo wajibu na kuacha yaliyo haramu ni sababu za kuingia Peponi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)