Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-58259

kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «كل مُسْكِرٍ خَمْرٌ، وكل مُسْكِرٍ حرام، ومن شرِب الخمر في الدنيا فمات وهو يُدْمِنُهَا لَمْ يَتُبْ، لَمْ يَشْرَبْهَا في الآخرة».

Tafsiri ya Kiswahili

kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- "kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"

English translation

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Every intoxicant is Khamr (alcoholic drink), and every intoxicant is prohibited. Whoever drinks Khamr in this world and dies while being addicted to it without repenting will not drink it in the Hereafter."

Maelezo

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kila kinachoondosha akili na kuiondoa hicho ni pombe yenye kulewesha, sawa iwe ni kunywa, au kula, au kuvuta kwa pumzi au vinginevyo, na kuwa kila kinacholevya na kuondoa akili Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiharamisha na amekataza, kiwe kidogo au kingi, Na kuwa kila mwenye kunywa aina yoyote ya vileo, na akaendelea kuvinywa, wala hakutubia mpaka akafa; Anastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnyima kuinywa Peponi.

Faida

  • Sababu ya kuharamishwa pombe ni kilevi, hivyo, kila chenye kulevya kiwe kwa aina yoyote ile ni haramu.
  • Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa imekusanya madhara na maovu makubwa.
  • Kunywa pombe peponi ni katika ukamilifu wa ladha na utimilifu wa neema.
  • Ambaye hakuizuia nafsi yake na unywaji pombe duniani Mwenyezi Mungu atamharamishia kuinywa peponi, kwani malipo huendana na matendo.
  • Hili ni himizo la kufanya haraka kutubia dhidi ya madhambi kabla ya kifo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)