Kulingania Dini na Kujitolea
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1852

Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni

Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya

Kiarabu

عن عرفجة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ، يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ، أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ، فَاقْتُلُوهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Farja -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni".

English translation

‘Arfajah (may Allah be pleased with him) reported: I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "If someone comes to you seeking to undermine your solidarity or disrupt your unity when you have agreed on one man, kill him."

Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa waislamu watakapokubaliana juu ya kiongozi mmoja, na mshikamano mmoja, kisha akaja anayetaka kumpokonya madaraka, au akataka kuwasambaratisha waislamu kuwafanya kuwa makundi makundi, ni lazima wamzuie na wampige vita, kwa kuzuia shari yake, na kwa kuhifadhi damu za waislamu.

Faida

  • Ulazima wa kumtii kiongozi anayesimamia mambo ya waislamu, katika mambo yasiyokuwa maasi, na uharamu wa kujitoa dhidi yake.
  • Atakayejitoa kwa kiongozi wa waislamu na umoja wao, basi ni wajibu kumpiga vita vyovyote vile itakavyokuwa nafasi yake ya cheo au ukoo.
  • Himizo la kuwa wamoja na kutofarakana na kuhitilafiana.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)