Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 1165

Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَنْظُرُ اللهُ إِلَى رَجُلٍ أَتَى رَجُلًا أَوِ امْرَأَةً فِي دُبُرٍ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma".

English translation

Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Allah does not look at a man who approaches a man or a woman anally."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ahadi kali ya adhabu kuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama mtazamo wa huruma mwanaume aliyemuingilia mwanaume mwenzake katika utupu wake wa nyuma, au mwanamke katika utupu wake wa nyuma, nakuwa hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.

Faida

  • Mwanaume kumwendea mwanaume mwenzake (Ulawiti) ni katika madhambi makubwa.
  • Kumwendea mwanamke katika tupu yake ya nyuma ni katika madhambi makubwa.
  • "Hamtazami Mwenyezi Mungu" Yaani: Mtazamo wa huruma au upole, na si makusudio yake: Kutazama kwa ujumla; kwa sababu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka hakuna chochote kinachofichikana kwake na hakitoweki machoni mwake chochote.
  • Matendo haya ni katika machafu makubwa na ni hatari sana kwa binadamu; kwakuwa ndani yake kuna kwenda kinyume na maumbile salama ya kibinadamu, na kupungua kwa kizazi, na kuharibu maisha ya ndoa, na kupandikiza uadui na chuki, na kuingia katika maeneo machafu yenye kutia kinyaa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)