Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. HE-58066

Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن أبي موسى رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لا نِكَاحَ إِلّا بِوَليٍّ».

Tafsiri ya Kiswahili

Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".

English translation

Abu Mūsa al-Ash‘ari (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There is no marriage except with a guardian."

Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwanamke haikubaliki ndoa yake ila kwa walii atakayesimamia kufungwa kwa ndoa.

Faida

  • Walii ni sharti la kusihi ndoa, ikifanyika bila walii, au mwanamke akajiozesha mwenyewe, haikubaliki.
  • Walii ni ndugu wa karibu wa kiume kwa mwanamke, asiozeshwe na walii wa mbali akiwepo walii wa karibu yake.
  • Ni sharti kwa walii: Awe mtu mzima (Aliyebalehe), mwanaume, na uwezo wa kupambanua na kujua masilahi ya ndoa, na wawe katika dini moja, msimamizi na msimamiwa, asiyekuwa na sifa hizi hastahiki kuwa msimamizi wa kufungisha ndoa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)