Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 726

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَرَأَ فِي رَكْعَتَيِ الْفَجْرِ: {قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ}، وَ{قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ}.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}.

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) recited: {Say, “O disbelievers”} and {Say: “He is Allah, the One”} in the two Rak‘ahs of Fajr.

Maelezo

Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akipenda kusoma katika rakaa mbili za sunna ya Alfajiri baada ya suratul-Fatiha, katika rakaa ya kwanza (Qul-yaa ayyula-kaafiruun), na katika rakaa ya pili suratul (Qul-huwallaahu ahad).

Faida

  • Kupendeza kusoma sura hizi mbili baada ya suratul Fatiha katika swala ya sunna ya Alfajiri.
  • Sura hizi mbili zinaitwa suratul-Ikhalswi (Utakasifu); kwa sbaabu katika suratul Kafirun kuna kujiweka mbali na yote wanayoyaabudu washirikina kinyume na Mwenyezi Mungu, nakuwa wao pia si waja wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ushirikina wao unaporomosha matendo yao, nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa, na ni kwa sababu katika suratul-Ikhlaswi kuna kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutakasa matendo kwa ajili yake na kubainisha sifa zake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)