Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ وَائِل بن حُجرٍ رضي الله عنه قَالَ: صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَانَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ»، وَعَنْ شِمَالِهِ: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Waili bin Hujari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah".
English translation
Wā’il ibn Hujr (may Allah be pleased with him) reported: I prayed with the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), and he used to make Taslīm (salutation of peace ending the prayer) to his right saying: "May Allah's peace, mercy, and blessings be upon you," and to his left saying: "May Allah's peace and mercy be upon you."
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumaliza swala yake anatoa salaam kuliani kwake na kushotoni kwake kwa kugeuka kwa uso wake upande wa kulia, pamoja na kusema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na anatoa salaam kushotoni kwake, kwa kugeuza uso wake upande wa kushoto, pamoja na kusema: "Assalaam alaiku warahmatullah".
Faida
- Sheria ya kutoa salaam mbili ndani ya swala, nakuwa salam hizo ni katika nguzo zake.
- Inapendeza kuleta ziada ya kauli "wabarakaatuh", katika baadhi ya nyakati; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa anadumu nayo.
- Kutamka salaam mbili ndani ya swala ni nguzo ya wajibu, na ama kitendo cha kugeuka wakati wa kuzitamka ni sunna.
- Inatakiwa iwe kauli ya: "Assalaam alaikum warahmatullaah" wakati wa kitendo cha kugeuka na si kabla yake wala baada yake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.