Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sunan an-Nasa'i · Na. HE-8905

Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم الرجل يلبس لِبْسَةَ المرأة، والمرأة تلبس لِبْسَةَ الرجل.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) cursed the man who wears women's clothes and the woman who wears men's clothes.

Maelezo

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu kwa kila mwanaume atakayejifananisha na mwanamke katika mavazi maalumu kwa ajili ya wanawake; sawa sawa iwe katika muonekano au rangi au jinsi au namna ya uvaaji na kujipamba. Au kwa mwanamke kujifananisha na mavazi maalumu kwa wanaume vile vile, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.

Faida

  • Amesema Shaukani: Kumeharamishwa wanawake kujifananisha na wanaume na wanaume kujifananisha na wanawake; kwa sababu laana huwa haiwi ila kwa kufanya jambo lililoharamishwa.
  • Amesema bin Uthaimiin: Zile wanazoshirikiana kati yao, mfano kama jezi au shati ambazo wanazivaa wanaume na wanawake hizi hazina tatizo, yaani hakuna tatizo akizivaa mwanaume na mwanamke; kwa sababu wanashirikiana.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)