Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ وَلَبِسَ خُفَّيْهِ فَلْيُصَلِّ فِيهِمَا، وَلْيَمْسَحْ عَلَيْهِمَا ثُمَّ لَا يَخْلَعْهُمَا إِنْ شَاءَ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokewa kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba".
English translation
Anas (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "If any of you makes ablution and puts on his leather socks, let him pray while having them on, and let him wipe over them without taking them off, if he wishes, except in the state of Janābah (major ritual impurity)."
Maelezo
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu atakapovaa khofu zake baada ya kutawadha, kisha akatengukwa udhu baada ya hapo, na akataka kutawadha, basi anatakiwa afute juu yake akitaka kufanya hivyo, na aswali nazo wala asizivue kwa muda maalum, isipokuwa atakapopatwa na janaba hapo atalazimika kuvua khofu na kuoga.
Faida
- Hairuhusiwi kufuta juu ya khofu mbili isipokuwa baada yakuwa na twahara kamili.
- Muda wa kufuta kwa mkazi: Ni mchana na usiku (Masaa 24), na kwa msafiri: Ni michana mitatu na usiku wake (Masaa 72).
- Kufuta juu ya Khofu mbili kunahusu tu hadathi ndogo nasi kubwa, ama hadathi kubwa haitakiwi kufuta, bali ni lazima kuvua khofu mbili na kuosha miguu miwili.
- Ni sunna kuswali na viatu na khofu na mfano wake na hii ni kwa sababu ya kwenda kinyume na Mayahudi, na hii ni pale viatu vitakapokuwa twahara (visafi), na havina udhia kwa wenye kuswali, au msikiti, mfano kama miskiti iliyotandikwa mabusati mtu hatakiwi kuswali navyo.
- Kufuta juu ya khofu mbili kuna urahisi na wepesi kwa umma huu.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.