“Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako?
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ؟ فَيَقُولُونَ: لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ، فَيَقُولُ: هَلْ رَضِيتُمْ؟ فَيَقُولُونَ: وَمَا لَنَا لاَ نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ؟ فَيَقُولُ: أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ، قَالُوا: يَا رَبِّ، وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟ فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي، فَلاَ أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".
English translation
Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Allah Almighty will say to the dwellers of Paradise: 'O people of Paradise!' They will reply: 'O our Lord, we present ourselves and are at Your pleasure.' He will say: ‘Are you contented?’ They will say: 'How could we not be contented, O Lord, when You have given us what You have not given to any of Your creation?' He will say: 'I shall give you something better than that?’ They will say: 'O Lord, what could be better than that?' He will say: 'I shall bestow My pleasure upon you and I shall not be displeased with you ever after that.'"
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Peponi wakiwa humo: Enyi watu wa Peponi, nao watamjibu kwa kusema: Labeka, tumekuitikia Mola wetu Mlezi! na utukufu ni wako, Atasema kuwaambia: Je! mmeridhika? Watasema: Ndiyo, tumeridhika; Kwa nini tusiridhike wakati umetupa ambacho hukumpa kiumbe wako yeyote! Atasema Mtukufu: Je, nisikupeni kilicho bora kuliko hicho? Watasema: Ewe Mola Mlezi, na ni kitu gani kilicho bora kuliko hicho? Atasema: Ninakuteremshieni juu yenu radhi zangu daima; na sitokukasirikieni baada yake milele.
Faida
- Mazungumzo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na watu wa peponi.
- Habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wa peponi ya kuwaridhia, na kuwateremshia radhi juu yao na kutochukia tena milele.
- Kila mtu Peponi ataridhika na hali yake licha ya kutofautiana viwango vyao na kupishana daraja zao; Kwa sababu wote walijibu kwa neno moja, ambalo ni: "Umetupa kile ambacho hukumpa yeyote katika viumbe vyako."
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.