Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-6762

Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ الْجُهَنِيِّ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَقْبَلَ إِلَيْهِ رَهْطٌ، فَبَايَعَ تِسْعَةً وَأَمْسَكَ عَنْ وَاحِدٍ، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، بَايَعْتَ تِسْعَةً وَتَرَكْتَ هَذَا؟ قَالَ: «إِنَّ عَلَيْهِ تَمِيمَةً»، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فَقَطَعَهَا، فَبَايَعَهُ، وَقَالَ: «مَنْ عَلَّقَ تَمِيمَةً فَقَدْ أَشْرَكَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Ukba Bin Aamir Al Juhaniy -Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuja kwake kundi, akawaunga mkono watu tisa na akamuacha mmoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewaunga mkono watu tisa na ukamuacha huyu? akasema: "Huyo yuko na hirizi", akaingiza mkono wake akaikata, akamuunga mkono, akasema: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina"

English translation

‘Uqbah ibn ‘Āmir al-Juhani (may Allah be pleased with him) reported: A group of people came to the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him). He accepted the pledge of allegiance of nine and did not accept it from one. They said: O Messenger of Allah, you accepted the pledge of nine but not of this one. He said: "He is wearing an amulet." So, he put his hand in and cut it, and thus, accepted his pledge and said: "Whoever hangs an amulet has committed Shirk (polytheism)."

Maelezo

Walikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na idadi yao walikuwa kumi, akawaunga mkono tisa miongoni mwao juu ya Uislamu na kufuata sheria, na hakumuunga mkono wa kumi, alipoulizwa kuhusu sababu yake, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo kavaa hirizi, nayo ni kila kinachotundikwa, ikiwemo shanga na vinginevyo kwa lengo la kuzuia kijicho au madhara. Yule bwana akaingiza mkono wake mahali ilipo hirizi na akaikata na akaepukana nayo, hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuunga mkono, na akasema akitahadharisha kuhusu hirizi na akibainisha hukumu yake: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya shirki".

Faida

  • Atakayemtegemea asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atampeleka kinyume na lengo lake.
  • Kuamini kuwa kutundika hirizi ni miongoni mwa sababu za kuzuia udhia wa kijicho, ni shirki ndogo, na ama akiitakidi kuwa inamnufaisha yenyewe, hii ni shirki kubwa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)