Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 3005

Kusibaki katika shingo la mnyama bangili za shaba au kengele isipokuwa (ahakikishe) zimekatwa

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن أبي بَشير الأنصاري رضي الله عنه: أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، قَالَ: فَأَرْسَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَسُولًا -وَالنَّاسُ فِي مَبِيتِهِمْ-: «لَا يَبْقَيَنَّ فِي رَقَبَةِ بَعِيرٍ قِلَادَةٌ مِنْ وَتَرٍ أَوْ قِلَادَةٌ إِلَّا قُطِعَتْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Bashiri Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, anasema: Akatuma mjumbe Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na watu wakiwa mahali pao pa kulala: "Kusibaki katika shingo la mnyama bangili za shaba au kengele isipokuwa (ahakikishe) zimekatwa".

English translation

Abu Bashīr al-Ansāri (may Allah be pleased with him) reported: He was with the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) on one of his journeys, and he sent a messenger ordering: "There should not remain any necklace of string or any other kind of necklace around the necks of camels without being cut."

Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya safari zake, na watu wakiwa mahali pao pa kulala wanapopumzikia katika vipandwa vyao na mahema yao, akamtuma mtu kwenda kwa watu akawaamrishe wakate vikamba vinavyotundikwa kwa wanyama sawa sawa ziwe zimetokana na kamba ya upinde -kamba ya upinde, au kinginecho kama kengele au kiatu, na hii ni kwa sababu walikuwa wakitundika kwa kuogopa kijicho, wakaamrishwa kuvikata; kwa sababu havizuii kwao chochote, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Allah peke yake asiye na mshirika.

Faida

  • Uharamu wa kutundika makamba na kengele kwa ajili ya kuleta manufaa au kuzuia madhara; kwani hilo ni katika ushirikina.
  • Kufunga kengele isiyoambatana na itikadi, kwa ajili ya urembo, au kuongozea mnyama au kumfungia haina tatizo.
  • Uwajibu wa kukemea uovu kulingana na uwezo.
  • Uwajibu wa moyo kuambatana na Allah peke yake asiye na mshirika.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)