Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah)
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ اللهُ، لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Ka'bu bin Hatim -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah). Atatazama kuliani kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Kisha ataangalia kushotoni kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Na ataangalia mbele yake, na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Basi uepukeni Moto hata kama ni kwa nusu ya tende."
English translation
‘Adyy ibn Hātim (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There is none among you except that Allah will speak to him, with no interpreter between Him and him. He will look to his right and see nothing except what he has sent forth, and he will look to his left and see nothing except what he has sent forth. And he will look ahead of him and see nothing except Hellfire in front of him. So, protect yourselves from Hellfire even with half a date."
Maelezo
Alieleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa kila Muumini atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama peke yake, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atazungumza naye bila ya muwakilishi, na hakuna mkalimani baina yao wa kutafsiri maneno, hivyo atatazama kulia na kushoto kutokana na hofu kali, labda atapata njia ya kwenda ili aweze kuokolewa na moto uliombele yake. Akitazama upande ulioko kuliani kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mema, na akitazama kushotoni kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mabaya, na akitazama mbele yake hatoona isipokuwa moto, na hatoweza kuukwepa, kwani hakuna budi ni lazima apite juu daraja (Swirat). Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wekeni kinga kati yenu na moto, kama kutoa sadaka na matendo mema, walau kwa kitu kidogo kama nusu ya tende.
Faida
- Himizo la kutoa sadaka hata kama itakuwa ndogo, na kujipamba na mambo mazuri, na kuamiliana kwa upole na maneno laini.
- Ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake siku ya Kiyama, kiasi kwamba hapatokuwa na kizuizi kati yao, wala muwakilishi wala mkalimani, basi muumini achukue tahadhari asijekwenda kinyume na amri za Mola wake Mlezi.
- Ni lazima kwa mtu asidharau anachokitoa sadaka, hata kama ni kidogo, kwani ni kinga ya kutoingia motoni.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.