Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1914

Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِطَرِيقٍ وَجَدَ غُصْنَ شَوْكٍ عَلَى الطَّرِيقِ فَأَخَّرَهُ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ فَغَفَرَ لَهُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "While a man was walking on a path, he found a thorn branch on the road, so he put it aside. Allah, thus, thanked him and forgave him."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba siku moja kuna mtu mmoja alikuwa akitembea njiani akapita katika tawi mti wa miba likiwa barabarani likiwaudhi waislamu, akalivuta na akaliondosha njiani, basi Mwenyezi Mungu akamshukuru na akamsamehe.

Faida

  • Fadhila za kuondoa udhia njiani, na kwamba hilo ni sababu ya kuupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.
  • Kutodharau matendo mema hata yakiwa ni madogo.
  • Uislamu ni dini ya usafi na kulinda mazingira na amani ya jamii nzima.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)