Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-6270

Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ عَادَ مَرِيضًا، لَمْ يَحْضُرْ أَجَلُهُ فَقَالَ عِنْدَهُ سَبْعَ مِرَارٍ: أَسْأَلُ اللَّهَ الْعَظِيمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ أَنْ يَشْفِيَكَ، إِلَّا عَافَاهُ اللَّهُ مِنْ ذَلِكَ الْمَرَضِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".

English translation

Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him and his father) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever visits a sick person whose time of death has not yet come, and says seven times in his presence: 'As’alullāh al-‘azhīm Rabb al-‘arshi al-‘azhīm an yashfiyak (I ask Allah the Great, Lord of the great Throne, to cure you),' except that Allah will cure him of that sickness."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hakuna muislamu atakayemtembelea muislamu katika maradhi yake, ambaye muda wa mauti yake haujafika, kisha aliyekwenda kumtembelea akamuombea mgonjwa kwa kusema: "Namuomba Allah Mtukufu" katika dhati yake na sifa zake na vitendo vyake, "Mola wa Arshi Tukufu akuponye", na akarudia mbele yake mara saba, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kutokana na maradhi hayo.

Faida

  • Inapendeza kumuombea mgonjwa kwa dua hii, na kuirudiarudia mara saba.
  • Kupatikana kwa ponyo kwa atakayeombewa mbele yake dua hii kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikisomwa kwa dhati na kwa mtu mwema.
  • Ataisoma dua hii kwa siri na kwa wazi, yote hiyo inafaa, lakini akimsikilizisha mgonjwa ndiyo bora zaidi; kwa sababu katika hilo kuna kuingiza furaha kwake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)