Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2695

Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَاللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "To say 'subhān Allah wa al-hamdulillāh wa lā ilāha illa Allah wa Allāhu akbar (Glory be to Allah, praise be to Allah, there is no god but Allah, and Allah is the Most Great)' is more beloved to me than everything upon which the sun rises."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kumtaja Allah Mtukufu kwa maneno haya matukufu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na utajo huo ni kusema: "Sub-haana llaah": Ni kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na mapungufu. "Alhamdulillaah": Ni kumsifia kwa sifa za ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Laa ilaaha illa llaah": Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Allaahu Akbaru: Mkubwa na Mtukufu kuliko kila kitu.

Faida

  • Himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hilo linapendeka zaidi kuliko vyote vilivyochomozewa na jua.
  • Himizo la kukithirisha dhikiri; kwakuwa ndani yake kuna malipo na fadhila kubwa.
  • Starehe za dunia ni ndogo na matamanio yake ni yenye kuondoka.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)