Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1623

Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani siwezi kushuhudia dhulma

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضيَ اللهُ عنهُما: أَنَّ أُمَّهُ بِنْتَ رَوَاحَةَ سَأَلَتْ أَبَاهُ بَعْضَ الْمَوْهِبَةِ مِنْ مَالِهِ لِابْنِهَا، فَالْتَوَى بِهَا سَنَةً ثُمَّ بَدَا لَهُ، فَقَالَتْ: لَا أَرْضَى حَتَّى تُشْهِدَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى مَا وَهَبْتَ لِابْنِي، فَأَخَذَ أَبِي بِيَدِي وَأَنَا يَوْمَئِذٍ غُلَامٌ، فَأَتَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ أُمَّ هَذَا بِنْتَ رَوَاحَةَ أَعْجَبَهَا أَنْ أُشْهِدَكَ عَلَى الَّذِي وَهَبْتُ لِابْنِهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا بَشِيرُ، أَلَكَ وَلَدٌ سِوَى هَذَا؟» قَالَ: نَعَمْ، فَقَالَ: «أَكُلَّهُمْ وَهَبْتَ لَهُ مِثْلَ هَذَا؟» قَالَ: لَا، قَالَ: «فَلَا تُشْهِدْنِي إِذن، فَإِنِّي لَا أَشْهَدُ عَلَى جَوْرٍ»، ولِمُسْلِمٍ: «فَأَشْهِدْ عَلَى هَذَا غَيْرِي».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Allah ziwe kwao yeye na baba yake: Ya kwamba mama yake bint Rawaha alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake anazompa mwanaye, akasitisha kutoa kwa mwaka mzima, kisha akaona amjibu, akasema (Mama Nuuman): Siwezi kuridhika mpaka umfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa shahidi kwa hivyo ulivyomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akamuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa mtoto huyu, binti Rawaha kapenda nikufanye wewe kuwa shahidi kwa zawadi nilizomzawadia mwanaye, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Bashiri una mtoto zaidi ya huyu?" Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wanao wote umewazadia kama huyu?" Akasema: Hapana. Akasema: "Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani siwezi kushuhudia dhulma", na kwa Imamu Muslim: "Kamtake ashuhudie mtu mwingine asiyekuwa mimi".

English translation

An-Nu‘mān ibn Bashīr (may Allah be pleased with him and his father) reported: His mother, Bint Rawāhah, asked his father for some of his wealth as a gift for her son. He hesitated for a year, but then he decided. She said: I will not be satisfied until you make the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) witness what you have given to my son. So, my father took my hand, and I was a young boy at that time, and he went to the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him). He said: O Messenger of Allah, the mother of this, Bint Rawāhah, wishes for you to witness what I have given as a gift to her son. The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "O Bashīr, do you have children other than this one?" He said: Yes. He then said: "Have you given them all the same gift as this?" He said: No. he said: "Then do not make me a witness, for I do not bear witness to injustice." And in the version of Muslim: "Then have someone else witness it, not me."

Maelezo

Ameeleza Nuuma bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba mama yake Amra binti Rawaha radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake kwa mwanaye, akawa mzito, na akachelewa kumjibu kwa muda wa mwaka mzima, kisha akaona amjibu swali lake, akamhofia mwanaye Nuuman, akasema: Siridhii mpaka umfanye kuwa shahidi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kile ulichomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akumuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa kijana huyu, binti Rawaha kapendezwa nikufanye kuwa shahidi kwa kile nilichomzawadia mwanaye, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Bashiri, je, una mtoto mwingine asiyekuwa huyu? Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wote umewazawadia mfano wa huyu. Akasema: Hapana. Akasema: Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani mimi sishuhudii upendeleo na dhulma. Na kwa Muslim alisema kwa kumkemea: Lakini mshuhudishe katika dhulma hii mwingine asiyekuwa mimi.

Faida

  • Ulazima wa kufanya uadilifu kati ya watoto wa kiume na wa kike katika vipawa na zawadi, ama matumizi yanakadiriwa kulingana haja na kila mmoja kwa uhitaji wake.
  • Kuwapendelea baadhi ya watoto na kuwaacha wengine ni katika dhulma, na wala haifai kulishuhudia hilo sawa sawa iwe kwa niaba au mtu mwenyewe.
  • Amesema Nawawi: Ni lazima mtu afanye uadilifu baina ya watoto wake katika zawadi, na amzawadie kila mmoja wao mfano wa alichomzawadia mwingine, na asipendelee, na afanye usawa kati ya mtoto wa kiume na wa kike, na wamesema baadhi ya watu wetu: Mtoto wa kiume anakuwa na mfano wa mafungu ya wanawake wawili, na kilicho sahihi nikuwa afanye usawa baina yao kwa mujibu wa hadithi hii.
  • Hukumu zote zinazofanyika kinyume sharia zinabatilika na wala hazitekelezwi.
  • Hakimu au mufti kutaka ufafanuzi kutoka kwa muulizaji katika yale yanayohitaji ufafanuzi; kwa mujibu wa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Je umefanya hivi kwa wanao wote?"
  • Amesema Nawawi: Na hapa kuna: Kufaa mzazi kurudia zawadi yake kwa mwanaye.
  • Amri ya kufanya yale yanayopelekea kuleta upendo baina ya ndugu, na kuacha yanayotia chuki baina yao, na kupandikiza chuki kwa wazazi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)