Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi
Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu
Kiarabu
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «من اقتبَسَ علْمًا مِنَ النُّجُومِ اقْتبَسَ شُعبَة مِن السِّحرِ، زادَ ما زادَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
English translation
Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Whoever acquires a branch of the knowledge of astrology acquires a branch of magic, of which he acquires more as long as he continues to do so."
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- yakuwa atakayejifunza na akachukua katika elimu ya nyota na mashukio yake na kutumia harakati zake kama ushahidi wa matukio ya ardhini kama kifo cha mtu fulani au uhai wake au maradhi yake, na mfano wake katika yatakayotokea siku za mbeleni, basi atakuwa kajifunza sehemu ya uchwi, nakuwa kadiri mwanadamu anavyokithirisha elimu hii basi anakithirisha uchawi.
Faida
- Uharamu wa unajimu ambao ni kueleza mambo yajayo kwa kutegemea hali za nyota; hili kwa sababu ni katika kudai elimu ya ghaibu.
- Kwa hakika unajimu ulioharamishwa ni katika aina za uchwi zinazopingana na tahuhidi, tofauti na kuzitazama nyota kwa ajili ya kujua uelekeo au kibla au kuingia kwa msimu na miezi haya ni halali.
- Kila anavozidisha katika kujifunza ndivyo anavyozidi kujifunza sehemu ya uchawi.
- Nyota zinafaida tatu amezitaja Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake: Ni pambo la mbingu, na ni alama hutumika kuongozea, na kipigo kwa mashetani
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.