Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-5981

Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن عمران بن حصين رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «‌لَيْسَ ‌مِنَّا ‌مَنْ ‌تَطَيَّرَ أَوْ تُطُيِّرَ لَهُ، أَوْ تَكَهَّنَ أَوْ تُكُهِّنَ لَهُ، أَوْ سَحَرَ أَوْ سُحِرَ لَهُ، وَمَنْ عَقَدَ عُقْدَةً، وَمَنْ أَتَى كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".

English translation

‘Imrān ibn Husayn (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "He is not one of us who seeks bad omens or has it done for him, or who practices soothsaying or has it done for him, or who practices sorcery or has it done for him; and whoever ties a knot, and whoever goes to a soothsayer and believes in what he says has disbelieved in what was revealed to Muhammad (may Allah's peace and blessings be upon him)."

Maelezo

Katoa onyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa atakayefanya baadhi ya matendo katika umma wake kwa kauli yake: "Si miongoni mwetu" Miongoni mwayo: La kwanza: "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa" Na asili ya hili: Ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi kama safari au biashara au mengineyo, akiruka upande wa kulia anajipa matumaini na anaendelea na analolitaka, na akirukia upande wa kushoto anaamini ni mkosi anaacha alichokikusudia, haifai kufanya hivi au kumlipa mwenye kumfanyia hivi, na inaingia hapa kupiga bao kwa kitu chochote sawa sawa chenye kusikika au kuonekana, kama ndege au wanyama au wenye ulemavu au namba au siku au mengineyo. La pili: "Atakayefanya ukuhani au akafanyiwa" Atakayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kwa kutumia nyota na vinginevyo, au akaja kwa anayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kama kuhani na mfano wake, akamsadikisha kwa yale ayasemayo kwa kudai kwake kujua elimu ya ghaibu, basi atakuwa kakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake. La tatu: "Atakayeroga au akarogewa" Naye ni yule atakayefanya uchawi yeye mwenyewe, au akampa kazi atakayemfanyia uchawi; ili amnufaishe yeyote au amdhuru, au akafunga fundo lolote kwa kufunga na nyuzi na kuzirogea kwa kusoma kinga za kishirikina zilizoharamishwa na akazipuliza.

Faida

  • Uwajibu wa kumtegemea Allah na kuamini hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, na kuharamishwa kwa imani za mikosi na nuksi na uchawi na ukuhani, au kuwauliza wenye mambo hayo.
  • Kudai kujua elimu ya ghaibu ni katika shirki inayopingana na tauhidi.
  • Uharamu wa kuwasadikisha makuhani na kuwaendea, na vinaingia hapa kusoma viganja na kusoma yaliyoandikwa kwenye vikombe na kutazamia nyota na, hata kama ni kwa kutaka kujua.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)