Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 15

Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن أنس رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote".

English translation

Anas (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "None of you truly believes until I become dearer to him than his father, his children, and all people."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu hawezi kua na imani kamili mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuliko mapenzi ya mama yake na baba yake na kijana wake wa kuime na wa kike na watu wote, na mapenzi yanaambatana na kumtii na kumtetea, na kuacha kumuasi.

Faida

  • Uwajibu wa kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na kutanguliza mapenzi yake kuliko mapenzi ya viumbe wote.
  • Katika alama za ukamilifu wa mapenzi: Ni kuzitetea sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kutoa nafsi na mali katika hilo.
  • Kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kunaendana na kumtii katika yale aliyoyaamrisha na kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza na kuyaepuka yale aliyoyakataza na kuyakemea, na kumfuata na kuacha uzushi.
  • Haki ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kubwa na ni ya mkazo kuliko watu wote; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya sisi kuongoka kutoka katika upotevu na kutuokoa na moto na kufuzu kuipata Pepo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)