Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2243

Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن أبي الهيَّاج الأسدي قال: قَالَ لِي ‌عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ: أَلَا أَبْعَثُكَ عَلَى مَا بَعَثَنِي عَلَيْهِ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ أَنْ لَا تَدَعَ تِمْثَالًا إِلَّا طَمَسْتَهُ، وَلَا قَبْرًا مُشْرِفًا إِلَّا سَوَّيْتَهُ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abul Hayyaji A-Asady amesema: Ally bin Abii Twalib alisema kuniambia: Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha.

English translation

Abu al-Hayyāj al-Asadi reported: 'Ali (may Allah be pleased with him) said to me: "Shall I not send you with the same instructions as the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) sent me with? Do not leave any statue without blotting it out or any raised grave without leveling it."

Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwatuma Masahaba wake wasiache "Sanamu" nayo ni picha ya kiumbe hai yenye kiwiliwili- isipokuwa wameliondoa au kuifuta. Na wasiache kaburi lililonyanyuka ila wamelisawazisha na ardhi, na wayabomoe yaliyomo katika majengo, au walisawazishe lisinyanyuliwe sana kupita usawa wa ardhi, bali linyanyuliwe kiasi cha shibri moja (kipimo cha kiganja).

Faida

  • Uharamu wa kuvipiga picha viumbe hai; kwa sababu hilo ni njia za kuelekea katika ushirikina.
  • Sheria ya kuondoa uovu kwa mkono kwa mwenye mamlaka au uwezo wa hilo.
  • Pupa ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuondoa mambo yote ambayo yana alama za enzi za ujinga, kama picha na vinyago na majengo yaliyo juu ya makaburi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)