Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 1586

Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ مَالِكِ بْنِ أَوْسِ بْنِ الْحَدَثَانِ أَنَّهُ قَالَ: أَقْبَلْتُ أَقُولُ مَنْ يَصْطَرِفُ الدَّرَاهِمَ؟ فَقَالَ طَلْحَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللهِ وَهُوَ عِنْدَ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضي الله عنهما: أَرِنَا ذَهَبَكَ، ثُمَّ ائْتِنَا، إِذَا جَاءَ خَادِمُنَا، نُعْطِكَ وَرِقَكَ، فَقَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: كَلَّا، وَاللهِ لَتُعْطِيَنَّهُ وَرِقَهُ، أَوْ لَتَرُدَّنَّ إِلَيْهِ ذَهَبَهُ، فَإِنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الْوَرِقُ بِالذَّهَبِ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yao wote: Tuonyeshe Dhahabu yako, kisha tuletee, atakapokuja mfanyakazi wetu tutakupa pesa yako, akasema Omari bin Khattwab: Hapana, ni lazima utampa haki yake, au umrejeshee Dhahabu yake, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono".

English translation

Mālik ibn Aws ibn al-Hadathān reported: I came saying: Who will exchange the dirhams? Talhah ibn ‘Ubaydullāh, who was in the company of ‘Umar ibn al-Khattāb (may Allah be pleased with both of them), said: Show us your gold, then come to us when our servant comes to give you your silver. Thereupon, ‘Umar ibn al-Khattāb said: No, by Allah, you must either give him his silver or give him back his gold, as the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Silver for gold is Riba (usury) unless exchanged on the spot; wheat for wheat is Riba unless exchanged on the spot; barley for barley is Riba unless exchanged on the spot; and dates for dates is Riba unless exchanged on the spot."

Maelezo

Taabii (Mwanafunzi wa Maswahaba) Malik bin Ausi anaeleza kuwa alikuwa na dinari za dhahabu, na alitaka kuzibadilisha kwa dirham za fedha, basi Twalha bin Ubaidillah (radhi za Allah ziwe juu yake) akamwambia: Tupe dinari zako nizione! Kisha akamwambia baada ya kuamua kununua: Njoo kwetu ikiwa mtumwa wetu atakuja baadaye tutakupe dirham za fedha, Omari bin Khattab Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alilaani aina hii ya muamala (biashara), na akaapa kwa Twalha kuwa atalipa fedha sasa, au amrudishie dhahabu yake aliyoichukua yeye, akasema kuwa kuuza fedha kwa dhahabu, au kinyume chake, lazima kupokea kuwe mkono kwa mkono, vinginevyo biashara hiyo itakuwa ni riba iliyoharamishwa na uuzaji batili, Dhahabu haiuzwi kwa fedha, wala fedha kwa dhahabu, isipokuwa mkono kwa mkono, na kufanyike kubadilishana, wala haiuzwi kwa ngano, na shayiri kwa shayiri, na tende kwa mfano wake, kipimo kwa kipimo, mkono kwa mkono; na haijuzu kuachana katika makubaliano kabla ya kuimiliki.

Faida

  • Kuna aina tano za vitu vilivyotajwa katika Hadith hii: dhahabu, fedha, ngano, shayiri, na tende Ikiwa uuzaji utafanyika katika kundi moja, masharti mawili lazima yatimizwe kwa ajili ya uhalali wake: kubadilishana katika kikao cha mkataba, na kufanana katika aina na uzito, kama vile dhahabu kwa dhahabu, vinginevyo itakuwa ni riba ya mkopo, na ikiwa ni tofauti mnavyouziana kama vile fedha na ngano kwa mfano, basi ili kusihi biashara hii linahitajika sharti moja wakati wa mkataba, vinginevyo itakuwa ni riba ya mkopo.
  • Makusudio ya kikao cha makubaliano: Ni mahala pa kuuziana, sawa sawa wawe wamekaa au wanatembea, au wamepanda, na makusudio ya kuachana ni kila namna ya kuachana waliyoizoea watu.
  • Katazo katika Hadithi linakusanya aina zote za dhahabu zilizosafishwa na ambazo hazijasafishwa, na aina zote za fedha, zilizosafishwa na zinginezo.
  • Miamala ya kifedha ya zama hizi ni wajibu kufanyika kilichowajibu katika biashara ya dhahabu na fedha, yaani endapo utataka kubadili fedha ya noti au sarafu kwa fedha nyingine ya noti au sarafu, kama Riyal kwa Dirham au Shilingi kwa Dollar, hapa inajuzu kupishana thamani kwa namna watakavyoelewana pande zote mbili, lakini ni wajibu kukabidhiana katika kikao cha mauziano, vinginevyo mauziano yatakuwa batili, na muamala huu utakuwa umeingia katika Riba iliyoharamishwa.
  • Miamala yote ya riba haifai, na makubaliano yake ni batili hata kama wataridhiana pande zote mbili; kwa sababu Uislamu unahifadhi haki ya mtu na ya Jamii nzima kwa ujumla, hata kama yeye mwenyewe atakubali haki yake iende.
  • Kukataza uovu na kuuzuia kwa atakayeweza kulifanya hilo.
  • Kutaja ushahidi wakati wa kukemea uovu, kama ilivyotokea kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)