Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sahih Muslim · Na. 2734

Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ اللهَ لَيَرْضَى عَنِ الْعَبْدِ أَنْ يَأْكُلَ الْأَكْلَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا، أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho".

English translation

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "Allah is pleased with one who eats some food and praises Him for it, or drinks some drink and praises Him for it."

Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa shukurani za mja kwa Mola wake Mlezi juu ya fadhila zake na neema zake ni miongoni mwa mambo ambayo huleta radhi za Allah; akala chakula akasema: Al-hamdulillah, na akanywa kinywaji na akasema: Al-hamdulillah.

Faida

  • Ukarimu wa Allah Mtukufu, ametoa fadhila zake kwa riziki na kisha akaridhia shukurani.
  • Radhi za Allah hupatikana kwa sababu nyepesi, kama kushukuru baada ya kula na kunywa.
  • Katika adabu za chakula na kinywaji: Ni kumshukuru Allah Mtukufu baada ya kula na kunywa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)