Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sahih Muslim · Na. 715

Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «الدُّنْيَا مَتَاعٌ، وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَةُ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema".

English translation

‘Abdullāh ibn ‘Amr (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The world is but an enjoyment and the best of worldly enjoyments is a righteous woman."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia na vyote vilivyomo si kingine isipokuwa ni kitu cha kustarehe nacho kwa muda mchache kisha kinaondoka, nakuwa starehe yake bora ni mke mwema, ambaye akimtazama anamfurahisha, na akimuamrisha anamtii, na akiwa mbali naye humuhifadhi ndani ya nafsi yake na mali yake.

Faida

  • Inafaa kustarehe na vizuri vya Dunia alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kupita kiasi au kujikweza.
  • Himizo la kuchagua mke mwema; kwa sababu ni msaada kwa mume katika kumtii Mola wake Mlezi.
  • Starehe bora ya Dunia ni ile itakayokuwa katika kumtii Allah au ikasaidia katika hilo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)