Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. HE-5792

Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا، وَخَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِنِسَائِهِمْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "The most perfect believer in terms of his faith is the one who has the most excellent manners, and the best of you are those who are best to their womenfolk."

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba mtu aliyekamilika zaidi kiimani ni yule itakayekuwa nzuri tabia yake, na hii kwa kuwa na uso mkunjufu, na kutenda mema, na maneno mazuri, na kuacha maudhi. Na muumini bora kuliko wote ni yule mbora kwa wake zake, kama mke wake na mabinti zake na dada zake na ndugu zake wengine wa kike; kwa sababu wao ndio watu wenye haki zaidi kutendewa tabia nzuri.

Faida

  • Ubora wa tabia njema nakuwa tabia njema ni katika imani.
  • Matendo ni katika imani, na imani huzidi na kupungua.
  • Heshima ya Uislamu kwa mwanamke na himizo la kumtendea wema.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)