Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. HE-5511

Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا جَلَسَ قَوْمٌ مَجْلِسًا لَمْ يَذْكُرُوا اللَّهَ فِيهِ وَلَمْ يُصَلُّوا عَلَى نَبِيِّهِمْ إِلاَّ كَانَ عَلَيْهِمْ تِرَةً، فَإِنْ شَاءَ عَذَّبَهُمْ وَإِنْ شَاءَ غَفَرَ لَهُمْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe".

English translation

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "No people sit in a gathering in which they do not remember Allah and do not invoke blessings upon their Prophet, except that it will be a source of regret for them. If He wills, He will punish them, and if He wills, He will forgive them."

Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hawatokaa watu katika kikao chochote na wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na wakawa hawakumsalia Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kikao hicho kitakuwa ni hasara na majuto juu yao na mapungufu siku ya Kiyama, akitaka atawaadhibu kwa madhambi yao yaliyotangulia na uzembe wao uliofuata, na akitaka atawasamehe ikiwa ni fadhila na rehema kutoka kwake.

Faida

  • Himizo la kufanya dhikiri na fadhila zake.
  • Fadhila za vikao ambavyo anatajwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na kumtaja Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakwamba vikao ambavyo havina hayo ni vikao vibaya kwa watu siku ya Kiyama.
  • Tahadhari iliyotajwa ya kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu haishii katika vikao pekee, bali inaenea katika sehemu zingine, amesema Nawawi: Ni machukizo kwa atakayekaa mahali aondoke bila kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake.
  • Masikitiko yatakayotokea siku ya Kiyama: Ima ni kwa sababu ya kupoteza malipo na thawabu kwa kutofaidika na wakati kwa kumtii Mwenyezi Mungu, na ima ni kwa madhambi na adhabu kwa kuutumia wakati kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.
  • Tahadhari hii ni pale kughafilika kutakapokuwa ni kwa mambo ya halali, je, ni vipi vikiwa vikao vya haramu ambavyo ndani yake kuna utesi na usengenyaji na mengineyo?!.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)