Qur'ani Tukufu na Fadhila Zake
SOMO · Sahih Muslim · Na. 789

Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka

Usomaji na Kufanyia Kazi Qur'ani

Kiarabu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّمَا مَثَلُ صَاحِبِ القُرْآنِ كَمَثَلِ صَاحِبِ الإِبِلِ المُعَقَّلَةِ، إِنْ عَاهَدَ عَلَيْهَا أَمْسَكَهَا، وَإِنْ أَطْلَقَهَا ذَهَبَتْ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka".

English translation

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The example of the companion of the Qur’an is like the owner of tied camels. If he keeps them tied, he will hold them; but if he releases them, they will run away."

Maelezo

Amemfananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyesoma Qur'ani na akakizoea kisomo chake sawa iwe kwa kutazama katika msahafu au kuhifadhi kwa moyo, na mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa kwa kamba ambazo hufungiwa wanyama, akimtazama mara kwa mara ataendelea kumshika na kumzuia, na akiacha kumfunga na kumtazama basi ataondoka na kutoroka, akianza kusoma Qur'ani msomaji wa Qur'ani basi huikumbuka, na asipoisoma basi ataisahau; madam kudumu kuisoma kutaendelea basi hifdhi yake itaendelea kubakia.

Faida

  • Himizo la kushikamana na Qur'ani na kuisoma, na tahadhari ya kutumbukia katika kuisahau.
  • Kudumu kuisoma Qur'ani huudhalilisha ulimi na huurahisishia kuisoma kwake, akiihama inakuwa nzito kwake na inampa tabu.
  • Amesema Kadhi: Na maana ya "Mwenye Qur'ani" Yaani: Aliyeizoea, na kusuhubiana: Ni kuzoea, na hukusudiwa: Fulani ni jamaa wa fulani, na watu wa peponi na watu wa motoni.
  • Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano.
  • Amesema bin Hajari: Na amemtaja ngamia pekee; kwa sababu ndio mnyama pekee anayetoroka haraka zaidi katika wanyama wafugwao na binadamu, na kumkamata kwake baada ya kutoroka ni kazi ngumu sana.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)